Gracious Amani: Alicia Keys afikiwa na video ya msichana kutoka Kenya, aguswa na kipaji chake

Gracious

Video ya msichana Mkenya kwa jina, Gracious Amani, kutoka eneo maskini nchini Kenya ambayo ilipata umaarufu kutokana na alivyouimba wimbo wa nyota wa muziki Alicia Keys hatimaye inaonekana kumfikia msanii huyo.

Alicia Keys ameipakia video hiyo katika ukurasa wake wa Twitter ulio na wafuasi 31 milioni, na kuambatisha ujumbe: "Look at this beautiful soul!! / Hebu tazama kiumbe huyu alivyo mzuri"

Alicia Keys

Chanzo cha picha, TWITTER

Amani mwenye miaka 13 alikuwa akiuimba wimbo kwa jina This Girl is on Fire na anasema aliuimba kama shukrani kwa mtalii aliyekuwa amempa yeye na watoto wenzake pipi.

Anasema hiyo ilikuwa ndiyo zawadi pekee ambayo angeweza kumpa mtalii huyo.

Video yake iliwekwa mtandaoni na mtalii huyo na mara moja ikawavutia wengi na kusambaa kwa kasi.

Amani anatoka mtaa wa Githurai Kimbo, Kiambu karibu na jiji la Nairobi.

Mtazame hapa:

Maelezo ya video, Msichana Mkenya aliyegusa nyoyo za wengi kwa kipaji chake.
Githu

Chanzo cha picha, Twitter

Githu

Chanzo cha picha, Twitter

Wanaomfuatilia Alicia Keys kwenye mtandao wa Twitter wamevutiwa sana video hiyo baadhi wakimsifu na pia kumshukuru msanii huyo kwa kuisambaza video hiyo.

Baadhi wamemtaka Keys kumfunza uimbaji au hata kuwa mdhamini wake na wengine wakashangaa kama ni yeye aliyemfunza uimbaji.

Alicia

Chanzo cha picha, TWITTER

Mandela Onchwati ameandika: "Natumai atafanikiwa, siku za usoni, tunaweza kuwa na hadithi ya ufanisi kutoka Githurai Ghetto Kenya. Nyota anayeibukia."

Rudy

Chanzo cha picha, Twitter

Huyu alitaka kutambuliwa, lakini Bob Marley alituacha zamani.

Alicia Keys

Chanzo cha picha, Twitter

Huyu anamuomba Alicia Keys amsaidie msichana huyo, lakini anasema ni miongoni mwa watu wenye vipaji kutoka Afrika wanaobanwa na sera za muda mrefu za kuibagua na kuifanya Afrika kusalia maskini.

Alicia Keys

Chanzo cha picha, TWITTER

Unaweza kusoma pia: