Benki ya Dunia: Mambo yanayochangia kilimo kutoufaidi uchumi Uganda

Uganda hupoteza kati ya asilimia 4 hadi 12 za mapato yake katika sekta ya Ukulima kulingana na ripoti ya benki ya dunia. Hasara hiyo hujiri kutokana na momonyoko wa udongo usidhiobitika ambao kwa kiasi kikubwa huathiri utaratibu.

Kulingana na ripoti hiyo hasara hiyo hutoa changamoto kubwa ambazo ni lazima zikabilwe ana kwa ana.

Mchango wa kilimo na mapato ya taifa kulingana na shirika la ubora wa bidhaa, ulianguka kwa asilimia 21 katika kipindi cha fedha cha mwaka 2017/18 ikilinganishwa na asilimia 21.5 katika kipindi cha bajeti cha mwaka 2016/17.

Kuanguka huko kumeendelea na kunakiliwa katika miaka mengine ya kifedha.

Kulingana na ripoti hiyo, Uganda imeathirika sana na mabadiliko ya hali ya hewa, ambayo hayaathiri pato pekee bali pia huwa na athari za muda mrefu za umasikini.

Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya Kampala, Mheshimiwa Christina Malmberg Calvo, meneja wa Benki ya Dunia nchini Uganda, alisema: "Chini ya asilimia 2 ya ardhi iliyopandwa imenyunyiziwa maji.

''Hivyobasi hii hapa ni hatua ya wazi. Kilimo cha Uganda kinapaswa kufanyiwa mabadiliko.

'Dhahabu ya kijani'

Kilimo, alisema, ni 'dhahabu ya kijani' ambayo inaweza kubadilisha uchumi. Hatahivyo, alijiuliza "kwa nini uwezo wa kilimo kizuri cha Uganda haujatambuliwa vizuri".

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, ukuaji wa kilimo na biashara unaweza kuonekana iwapo kuna ongezeko la ushiriki wa sekta binafsi na fedha.

Wakulima wadogo, Bi Malmberg anasema, wana haja ya kujiunga katika vyama na mashirika ya wazalishaji ili kushiriki kwa ufanisi zaidi na masoko ya kuuza mapato.

Dr Joseph Muvawala, mkurugenzi mtendaji wa Taifa wa halmashauri ya Mipango (NPA), alisema kuwa kuna shida na jinsi taasisi za Uganda zinavyofanya kazi, swala linalochangia pakubwa kufeli kwake.

Katibu wa kudumu katika wizara ya kilimo , bwana Pius Wakabi Kassaja, alisema Waganda wanapaswa kuhitimisha kilimo kutoka kuwa kitu cha kujifurahisha akidai kwamba ni wakati mzuri tunaangazia sera kuhusu kilimo endelevu.

Kilimo, alisema, lazima kiwe biashara ambayo inasimamiwa na sera za kibiashara kuhusu mahitaji na usambazaji.

Mambo matano yanayochangia kudorora kwa kilimo

  • Mambo matano yanayochangia kudorora kwa kilimo
  • Kudhoofika kwa taasisi za umma za kushinikiza ukuwaji wa kilimo.
  • Utepetevu katika matumizi ya umma kwenye sekta ya kilimo.
  • Ukosefu wa sheria na sera za kutosha za kilimo.
  • Ukosefu wa mali katika sekta hiyo inayoweza kutumiwa kuomba mkopo.
  • Ukame na wadudu waharibifu wa mimea.

Kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Uganda.

70% ya ajira nchini zinatokana na sekta hiyo na huchangia nusu ya mauzo ya taifa hilo katika masoko ya nje.

Kwasababu raia wengi Uganda huishi maeneo ya mashambani na hujishughulisha na ukulima, benki ya dunia inapendekeza kushinikiza biashara inayotokana na sekta hiyo.

Na hilo taasisi hiyo ya fedha inaeleza litasaidia kupunguza umaskini, kuimarisha ustawi na kuunda nafasi zaidi za ajira hususan kwa wanawake na vijana.

Kilimo Uganda kina nafasi kubwa ya ukuwaji na kugeuza uchumi wa taifa hilo na kina uwezo wa kuleta faida kubwa kwa wakulima wadogo, ripoti hiyo inasema.