Shule ya Moi Girls yafungwa Kenya baada ya tuhuma za kubakwa wasichana shuleni

Makundi ya kutetea haki za wanawake yanaandamana nje ya Shule Moi Girls Nairobi
Maelezo ya picha, Makundi ya kutetea haki za wanawake yanaandamana nje ya Shule Moi Girls Nairobi
Muda wa kusoma: Dakika 2

Je watoto katika shule za Mabweni wako salama kiasi gani? Hilo ndilo suali kubwa wanaouliza Wakenya baada ya kuibuka tuhuma za kubakwa kwa wasichana katika shule moja mjini Nairobi.

Shutuma kali zimeibuka nchini Kenya katika mitandao ya kijamii huku masuali mengi yakiulizwa kuhusu usalama wa watoto wanaosoma katika shule za mabweni baada ya tuhuma kwamba wasichana kadhaa katika shule moja ya upili Nairobi Kenya walibakwa na mtu asiyejulikana ndani ya shule hiyo Jumamosi usiku.

Makundi ya kutetea haki za wanawake yanaandamana nje ya Shule Moi Girls Nairobi kuitaka serikali ichukuwe hatua za kisheria dhidi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Wazazi waliokuwa na ghadhabu waliwasili katika shule ya upili ya Moi mjini Nairobi Jumapili asubuhi kuwachukua watoto wao kufuatia agizo la wizara ya elimu nchini.

Shule ya upili ya Moi Nairobi

Chanzo cha picha, Getty Images

Akizungumza na waandishi habari alipoizuru shule hiyo, waziri wa elimu nchini Amina Mohammed amesema uchunguzi utaendelea, na kwamba watachunguza mapengo yoyote yaliopo na wayashughulikie.

'Nataka niwahakikishie kwamba tutaimarisha usalama shuleni, na tutahakikisha kwamba watoto wetu wanapokuja hapa, watasoma kama walivyokuja kusoma', amesema Waziri Amina.

Kuna mzozo kuhusu idadi kamili ya wasichana wanaotuhumiwa kubakwa, huku ripoti za kukinzana zikitaja mischana mmoja nyingine zikitaja wasichana watatu ndio waliobakwa katika mkasa huo.

Gazeti moja nchini linasema msichana mmoja aliyeathiriwa amemtaja mwanamume - aliyemueleza kwa rangi ya ngozi mwilini kuwa ni wa kahawia - aliwashambulia usiku.

Waziri wa elimu Kenya Amina Mohammed amesema watachunguza mapengo yoyote yaliopo na wayashughulikie

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waziri wa elimu Kenya Amina Mohammed amesema watachunguza mapengo yoyote yaliopo na wayashughulikie

Afisa mkuu wa polisi anayelisimamia eneo ambako shule hiyo iko, amethibitisha kuwa msichana wa kidato cha pili alibakwa katika choo kilichoko nje ya bweni, lakini hakuweza kuthibitisha tuhuma kuhusu waathiriwa wengine wawili.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Hii sio mara ya kwanza kwa shule hiyo ya Moi Girls kujipata matatani.

Idara ya upelelezi nchini sasa inchunguza tuhuma hizo na kwamba maafisa wa shule hiyo waliwataka wanafunzi wanyamaze wasiripoti kisa hicho cha ubakaji.

Baadhi ya wazazi na wakaazi wa eneo la shule hiyo waliojitokeza kujaribu kuwajulia hali wanawao katika shule hiyo baada ya mkasa huo wa moto
Maelezo ya picha, Wazazi waliofika katika shule ya upili ya Moi kuwajulia watoto wao baada ya mkasa huo

Kuna tuhuma pia kwamba mwanafunzi huyo wa kidato chapili aliambiwa ajioshe baada ya mkasa huo , na kwamba aliahidiwa kupewa ufadhili wa karo ya shule.

Kwa sasa shule hiyo ya Moi Girls imefungwa kwa angalau wiki moja kuruhusu uchunguzi ufanyike.