Mwanamfalme Charles kumsindikiza Meghan kwenye madhabahu

Mwanamfalme Charles atamsindikiza Meghan Markle kwenye madhabahu kesho Jumamosi atakapoolewa na mwanamfalme Harry, kasri la Kensington limesema.

Babake bi Markle, Thomas, hatohudhuria harusi hiyo kwasababu amefanyiwa upasuaji wa moyo.

Mwanamfalme wa Wales ana "furaha ya kumkaribisha Bi Markle katika familia ya ufalme kwa namna hii", Kasri liliongeza.

Babu yake mwanamfalme Harry Duke wa Edinburgh, pia atahudhuria harusi hiyo, kasri la Buckingham limethibitisha.

Mwanamfalme Philip, mwenye umri wa miaka 96, amekuwa akipata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa paja lake.

Mamake bi Markle, Doria Ragland, atampeleka binti yake hadi katika kanisa la St George huko Windsor kutakako fanyika harusi hiyo.

Bi Ragland anakutana na nMalkia kwa mara ya kwanza leo katika kasri la Windsor akiandamana na Meghan, mwenye umri wa miaka 36, na Mwanamfalme Harry, aliye na umri wa miaka 33.

Ameshatambulishwa kwa Mwanamfalme Charles.

Akizungumza na BBC kutoka Windsor, Mwanahabari wa shirika la utanganzaji Marekani TMZ, Sean Mandell alisema amezungumza na babake Meghan Jumatano na kwamba 'aneandelea kupata nafuu baada ya upasuaji'.

Mandell - aliyeichapisha taarifa hiyo wa kwanza - amesema Bwana Markle alitambua Jumanne kwamba hatoweza kusafiri kuelekea Windsor.

Je harusi ya kifalme Uingereza inafuatiliwaje Afrika mashariki?

"Maumivu ya kifuani yalikuwa yanamzidi kutokana na kuzidiwa kwa hisia," alisema.

"Wakati madakttari walipomuambia kwamba anahitaji upasuaji , aliamua kufuata maagizo licha ya kwamba alitaka sana kuhuduhuria harusi ya Meghan,"alisema Mandell.

Bi Markle alitoa taarifa Alhamisi akisema anaomba babake apewe nafasi na faragha ili aiangalie afya yake.