Kwa Picha: Zaidi ya watu 40 wafariki mkasa wa bwawa Kenya
Watu zaidi ya 40 wamefariki baada ya bwawa moja kubwa katika shamba la kibinafsi eneo la Solai, Nakuru kaskazini magharibi mwa jiji la Nairobi kuvunja kingo zake.
Juhudi za uokoaji zinaendelea.

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Bwawa hilo lilivunja kingo zake baada ya kujaa kutokana na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha katika eneo hilo na maeneo mengine Kenya.
Watu zaidi ya 100 kufikia sasa wamefariki nchini Kenya kutokana na mafuriko ambayo yameathiri pia nchi jirani kama vile Tanzania, Uganda, Somalia na Ethiopia.

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya limekuwa likisaidia na maafisa wa huduma za dharura wa serikali na wahudumu wa kujitolea kuwasaidia waathiriwa.
Hapa chini ni baadhi ya wakazi walionusurika wakiwa ndani ya gari la kuwabebea wagonjwa.

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Bwawa hilo linapatikana eneo la Solai, wadi wa Kabazi kilomita 40 hivi kaskazini mwa mji wa Nakuru.









