Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa Picha: Mlipuko wa volkano 'wameza' nyumba za watu Hawaii, Marekani
Milipuko ya volkano katika eneo la Kilauea, Hawaii imeharibu zaidi ya nyumba 26 na inatishia kuharibu nyumba nyingine mamia kadha.
Nyufa mpya zilitokea usiku maeneo hayo. Tayari watu zaidi ya 2,000 wamehamishwa makwao.
Baadhi waliruhusiwa kurejea Jumapili kuokoa wanyama wao, lakini maafisa wa serikali wanasema eneo hilo si salama.
Nyufa na mashimo mapya yalizuka usiku mtaa wa Leilani. Matope yenye moto yalirushwa futi 230 (mita 70) hewani.
Kisiwa hicho kilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi la nguvu ya 6.9 katika vipimo vya Richter Ijumaa.
Kilauea ni moja ya volkano zinazolipuka zaidi duniani. Imekuwa ikilipuka kwa miaka 35 sasa.