Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ufa unaotoa dalili Tanzania na Kenya zinajitenga na Afrika
Wanasayansi wa miamba na ardhi wameonya ufa mkubwa uliotokea katika eneo la bonde la Ufa nchini Kenya ni ishara kuwa bara la Afrika linaweza kugawanyika katika vipande viwili miaka milioni 50 ijayo.
Sehemu ya barabara kuu inayopitia katika eneo hilo imezama ardhini na ufa huo umeenea hadi katika makazi ya watu ambao sasa wameanza kuhama wakihofia maisha yao.
Mwandishi wetu Ferdinand Omondi na Kenneth Mungai walizuru maeneo hayo na kuandaa taarifa ifuatayo.