Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Parachichi kutoka Hawaii ladaiwa kuwa kubwa zaidi duniani
Mwanamke katika jimbo la Hawaii, Marekani huenda amepata parachichi kubwa zaidi duniani, taarifa zinasema.
Pamela Wang kutoka eneo la Kealakekua katika kisiwa cha Big Island anasema alikuwa nje kwenye matembezi alipoliona tunda hilo la uzani wa kilo 2.35 (5.2lb).
"Lilikuwa kubwa kama kichwa changu," aliambia gazeti la West Hawaii Today.
Bi Wang amewasilisha ombi rasmi kwa Guinness World Records kutaka litambuliwe kama parachichi kubwa zaidi kuwahi kupatikana duniani.
Mwaka 2009 parachichi la kilo 2.18 (4.8lb) kutoka Venezuela lilitambuliwa rasmi kuwa kubwa zaidi duniani.
Bi Wang anasema tunda hilo lilitoka kwa mparachichi wa zaidi ya miaka 40 ambao umekuwa karibu na barabara
Jimbo la Hawaii, tunda ambalo linatoka kwa tawi lililoning'inia barabarani au linaloanguka barabarani linaweza kuchukuliwa na mtu yeyote yule na liwe lake.
Amewasilisha picha za tunda hilo kwa West Hawaii Today.
Bw Wang anatarajia kupata majibu kutoka kwa Guinness katika kipindi cha miezi miwili.
Anasema baada ya kulipima walilila tunda hilo kubwa na marafiki zake.
"Lilikuwa tamu sana. Mti huo ni mzuri sana. Tulikuwa watu 10 na hatukumaliza nusu ya parachichi hilo," anasema.