Kwa Picha: Mlipuko wa volkano 'wameza' nyumba za watu Hawaii, Marekani

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Nyufa zaidi zimetokea katika mitaa ya Leilani na kuharibu nyumba za watuMilipuko ya volkano katika eneo la Kilauea, Hawaii imeharibu zaidi ya nyumba 26 na inatishia kuharibu nyumba nyingine mamia kadha.
Nyufa mpya zilitokea usiku maeneo hayo. Tayari watu zaidi ya 2,000 wamehamishwa makwao.
Baadhi waliruhusiwa kurejea Jumapili kuokoa wanyama wao, lakini maafisa wa serikali wanasema eneo hilo si salama.
Nyufa na mashimo mapya yalizuka usiku mtaa wa Leilani. Matope yenye moto yalirushwa futi 230 (mita 70) hewani.
Kisiwa hicho kilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi la nguvu ya 6.9 katika vipimo vya Richter Ijumaa.
Kilauea ni moja ya volkano zinazolipuka zaidi duniani. Imekuwa ikilipuka kwa miaka 35 sasa.

Chanzo cha picha, USGS
Maelezo ya picha, Baadhi ya maeneo, nyufa zinazofuka moshi zilizuka
Chanzo cha picha, USGS
Maelezo ya picha, Matope ya volkano yakirushwa mitaa ya Makamae na Leilan
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Maafisa wanasema nyumba 26 zimeharibiwa kisiwani humo. Mamia zaidi zimo hatarini
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Nyufa kumi tofauti zimezuka maeneo ya karibu, eneo la umbali wa 40km kutoka kwenye shimo la katikati ya mlima Maelezo ya video, Matope ya volkano yanaendelea kumwagika kutoka kwa volkano ya Kilauea, Hawaii
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Baadhi ya wakazi waliruhusiwa kurejea kuwachukua wanyama wao baada ya kujaza fomu
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wengi wanaishi kwenye kambi ya muda. Hawajui wataruhusiwa kurejea lini
Chanzo cha picha, USGS
Maelezo ya picha, Volkano ya Kilauea ililipuka Ijumaa, baada ya tetemeko la nguvu ya 6.9
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Moshi wa volkano ukifuka kutoka kwa mlima Kilauea
Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Kilauea ni moja ya volkano zinazolipuka zaidi duniani. Imekuwa ikilipuka kwa miaka 35 sasa.Soma pia: