Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ali Kiba afunga ndoa na mpenziwe wa Kenya
Nyota wa muziki wa Bongo nchini Tanzania Ali Saleh Kiba ameuacha rasmi ukapera baada ya kufunga ndoa na mpenziwe kutoka Kenya.
Harusi hiyo ya kukata na shoka iliofanyika katika msikiti wa Ummul Kulthum ilihudhuriwa na rafiki wa mwanamuziki huyo Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.
Mwanamuziki huyo wa wimbo wa Seduce me aliisafirisha familia yake mjini Mombasa siku moja kabla ya kumuoa mchumba wake.
Ni watu wachache pekee walioalikwa katika harusi hiyo iliodaiwa kufanyika kisiri.
Duru zimearifu kwamba sherehe nyengine ya kukata na shoka inatarajiwa kufanyika Aprili 26 mjini Dar es Salaam.