Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Dalai Lama azindua programu tumishi ya iPhone
Dalai Lama amezindua programu tumishi ya simu kwa wafuasi wake kuweza kufuatilia kwa karibu kuhusu safari na mafunzo yake.
Kiongozi huyo wa kidini wa Tibet anayeishi uhamishoni mwenye umri wa miaka 82, ana akunti ya Twitter iliyo na wafuasi zaidi ya milioni 16.
App hiyo ya bure kwa sasa inapatikana kwenye simu za iPhone pekee, na ataitumia kutoa taarifa, video, picha na taarifa nyinginezo
Kuna programu nyinge tumishi za kidini zilizozinduliwa, zinazoruhusu viongozi kuwasiliana na wafuasi wao na kuwasiaidia watu kutafuta chakula kinachoambatana na dini zao, wanaposafiri.
App hiyo inaitwa, Dalai Lama, haijakaguliwa sana na watumizi.
The Dalai Lama
- Jina lake ni Tenzin Gyatso
- AlizaliwaTibet, amekuwa uhamishoni kwa miongo sita tangu Uchina ukandamize vuguvugu la Tibet
- Yeye ni Budda, anayetambulika kama mojawapo ya viongozi wakuu duniani na huhubiri amani na uvumilivu wa ki imani mara kwa mara
- Anashinikiza kujitawala kwa Tibet iliomo ndani ya China lakini utawala wa China unamuona kuwa mtu anayeshinikiza kugawanayika kwa nchi hiyo
- Mnamo 1989 alishinda tuzo ya Nobel ya amani
- BBC imeshinda kupata picha yake akiwa anatumia simu za kisasa 'smartphone'