Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ndege ya Urusi iliyotoweka yapatikana chini ya bahari Norway
Norway inasema kuwa kundi la watafutaji limepata mabaki ya ndege ya Urusi aina ya helikopta, ambayo ilianguka baharini ikiwa na watu 8 ndani yake.
Ndege hiyo ambayo haikuwa haijulikani iliko tangu Alhamisi, kwa sasa iko chini ya bahari karibu na eneo la Barentsburg, kwa mujibu wa maafisa.
Polisi nchini Norway sasa wanaweza kuwatafuta wale waliokuwa ndani ya ndege hiyo, taarifa hiyo ilisema.
Ofisi ya Urusi huko Barentsburg inasema kuwa wahudumu watano na wanasayansi watatu, walikuwa ndani ya ndege hiyo wote raia wa Urusi na kuna hofu kuwa wamefariki.
Ilikuwa katika safari fupi kutoka Pyramiden kwenda Barentsburg eneo la madini la Urusi.