Kim Jong-un ampandisha cheo dada yake mdogo

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, amempandisha cheo dada yake mdogo, na kumpa madaraka zaidi katika chama tawala cha wafanyakazi.

Kim Yo-jong, anayeaminika kuwa na umri wa zaidi ya miaka 26 amekuwa mjumbe katika kamati kuu ya chama, ambalo ni baraza kuu la uamuzi linalojulikana kama politburo.

Bi Kim Yo-jong alipewa kwanza wadhifa wa kuwa afisa wa wa cheo cha juu wa chama, miaka mitatu iliyopita.

Familia ya Kim, imeongoza Korea Kaskazini, tangu nchi hiyo ilipoundwa, mwaka wa 1948.