Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Polisi ya Tanzania yakana madai ya kumpeleleza Tundu Lissu
Jeshi la polisi nchini Tanzania limepinga ripoti zilizokuwa zikisambaa katika vyombo vya habari zikidai kwamba afisa wake mmoja yupo mjini Nairobi kumpeleleza Tundu Lissu.
Mbunge huyo alipigwa risasi karibu na nyumbani kwake mjini Dodoma tarehe 7 mwezi Septemba na watu wasiojulikana.
Anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya Aga Khan Jijini Nairobi ambako alisafirishwa kwa matibabu maalum.
Hatahivyo kulingana msemaji wa polisi Barnabas Mwakalukwa, ripoti kwamba jeshi la polisi lilituma afisa wake ili kumchunguza wakili huyo ni ya uwongo.
''Tunatekeleza wajibu wetu kulingana na sheria na tumeshangazwa na watu wanaotafuta umaarufu kupitia kuliharibia sifa jeshi la polisi'', alisema Mwakalukwa wakati wa mkutano na wanahabari.
Alisema kuwa ni uwongo kwamba afisa aliyetajwa alikuwa yuko Nairobi na kwamba alikuwa mjini humo kuendelea na mafunzo yalioanza Septemba 4 na kukamilika Septemba 8.
Afisa huyo tayari amerudi nyumbani Tanzania.