Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Coleen: Mke wa Wayne Rooney ni mjamzito tena
Mke wa mchezaji nyota wa England Wayne Rooney, Coleen, ni mjamzito tena.
Mwanamke huyo wa miaka 31 ametanagza habari hizo kwa wafuasi wake 1.25 milioni kwenye Twitter na kusema kwamba anaweza kuwatangazia watu kwani amepimwa na kuchunguzwa vyema.
Ameandika: "Nina furaha sana!!! ..... Sijawahi kukanusha habari hizi, lakini nilikuwa ninazilinda vyema!! Nimepimwa & na kuchunguzwa na kila kitu kiko sawa...Mtoto nambari 4 yupo njiani."
Wayne, ambaye aliyehamia klabu ya Everton msimu huu, alisambaza ujumbe huo.
Coleen na Wayne walifunga ndoa mwaka 2008 baada yao kuchumbiana wakiwa bado vijana wadogo Liverpool.
Wana watoto watatu wa kiume - Kai, wa miaka minane, Klay, wa miaka minne, na Kit, aliyezaliwa Januari 2016.
Coleen amezungumzia kuhusu hamu yake ya kutaka kujaliwa msichana miezi ya karibuni.
Katika mahojiano na jarida la New, alisema: "Nafikiria kuhusu kumpata msichana. Nina familia kubwa, kwa hivyo ningetaka wasichana sawa na ninavyowataka wavulana."
Coleen Rooney amesema wakati huu hatalila kondo la nyuma la mtoto wake kama alivyofanya baada ya kujifungua Kit.