CIA: Hakuna uwezekano wa kutokea vita vya nuklia na Korea Kaskazini

Chanzo cha picha, KCNA/AFP
Hakuna uwezekano wa tisho la kutokea vita vya nuklia na Korea Kaskazini, kwa mujibu wa mkugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani, licha ya kuongezeka kwa msukosuko.
Mike Pompeo alisema kuwa Korea Kaskazini inaendelea kwa kasi na mipango yake ya nuklia na jaribio lolote la kombora halitakuwa na kutia wasiwasi.
Lakini alionya kuwa uvumilivu wa Marekani unafikia kikomo.
Pande zote mbili zimetupiana maneno makali huku rais Donald Trump akitishia kuikabili vikali Korea Kaskazini.
Bwana Pompeo anasema ana uhakika kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un atajaribu kuendelea na mpango wa nuklia wa nchi hiyo.

Chanzo cha picha, AFP
Alipoulizwa kuhusu ni muda gani Korea Kaskazini wamebaki nayo kabla ya kuunda silaha ya nuklia ambayo inaweza kushambulia Marekani, alisema kuwa wako karibu.
Msukosuko wa siku nyinyi kuhusu mpango wa nukilia wa Korea Kaskazini uliongezeka zaidi wakati ilifanya jaribio la makomboa mawili ya masafa marefu mwezi Julai.
Hatua hiyo ilisababisha awamu nyingine ya vikwazo vya kiuchumi vya Umoja wa Mataifa hatua iliyoghadhabisha utawala wa Kim.
Trump alisema kuwa jeshi la la Marekani liko tarayi huku Korea Kaskania ikimlaumu kwa kuchochea vita katika rasi ya Korea.












