Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ndovu amuua mwelekezi wa safari Zimbabwe
Mwelekezi mmoja wa safari ameuwawa na ndovu baada ya ndovu kumfuata nchini Zimbabwe, kwa mujibu wa kampuni moja wa kitalii.
Kampuni ya Adventure Zone ilisema kuwa ndovu huyo anayefahamika kama Mbaje alimuua Enock Kufandanda siku ya Jumapili jioni.
Ilisema kuwa Bwana Kufandada alikuwa mfanyakazi mzuri aliyekjitolea na ambaye watamkosa sana.
Gazeti moja lilisema kuwa Kufandanda alikuwa ameenda kuwachukua ndovu ili kuwatembeza.
Ndovu huyo kwa sasa ameuwawa