Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maelfu waandamana dhidi ya Rais Erdogan Uturuki
Maelfu ya watu wameandama katika mji wa Istanbul nchini Uturuki dhidi ya Rais wa nchi hiyo Recip Tayyip Erdogan.
Akihutubia katika maandamano hayo, kiongozi mkuu wa upinzani Kemal Kilicdaroglu, ameishutumu serikali kwa mfululizo wa kukamatwa na kufungwa kwa watu ikiwa ni matokeo ya jaribio la mapinduzi lililoshindikana mwaka jana.
Amesema raia wa Uturuki wanaishi chini ya Udikteta.
Rais Erdogan maandamano hayo yanaunga mkono ugaidi.