Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kipindupindu chawaua watu 700 nchini Somalia
Watu zaidi 700 wamefariki kutoka na mlipuko wa kipindupindu nchini Somalia, kulingana na baraza la wakimbizi la Norway. Mlipuko huo unadaiwa kuwa miongoni mwa milipuko mibaya zaidi ya ugonjwa huo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Baraza hilo limesema Sudan Kusini pia imeripoti visa visivyo vya kawaida vya ugonjwa huo.
Watu wengi haswa watoto wamefariki kutokana na kipindupindu zaidi ya vita nchini Somalia.
Sudan Kusini imerekodi vifo 160 kutokana na ugonjwa huo, ambao huwa nadra katika msimu huu wa kiangazi.
Hakukuripotiwa kisa chochote cha kipindupindu katika msimu kama huu mwaka jana.
Baraza hilo la wakimbizi la Norway limesema vita ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa katika nchi hizo mbili vimeharibu sekta ya afya na mfumo ya maji safi na maji taka.
Katibu mkuu wa shirika hilo, Jan Egeland amesema kuna hitaji la dharura la kupata maji safi, huduma za afya na dawa ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.