China yazindua manowari mpya ya kijeshi

Chanzo cha picha, Reuters
China imezindua manowari mpya ya kijeshi iliyoundwa nchini humo katika jitihada za hivi punde za kuboresha jeshi lake.
Uzinduzi huo unajiri baada ya China kuzindua meli ya kwanza kuundwa nchini humo mwezi Aprili.
Licha ya kuwepo misukosuko kusini mwa habari ya China, China inachukua hatua kubwa katika eneo hilo la bahari ambao inadai kumiliki.
Manowari huyo yenye uzito wa tani 10,000 itafanyiwa majaribio makubwa.
China imeonyesha ubabe wake katika maeno inayodai kuwa yake kusini mwa bahari ya China baada ya Trump kuapa kuizuia China kumiliki eneo hilo.

Mara kwa mara Marekani imekuwa ikituma meli na ndege katika visiwa vinavyozozaniwa na kulitaja eneo hilo kuwa la kimataifa.
China, Vietnam, Uflilipino, Taiwan, Malaysia na Brunei wote wanadai sehemu hiyo. China imetetea madai yake kwa kujenga visiwa vilivyogharimu pesa nyingi na doria za kijeshi.
Wakati uchumi wake unazidi kuimarika, China inazidi kuboresha jeshi lake
Mwezi Machi ilitangaza kuwa itaongeza bajeti ya jeshi lake kwa karibu asilimia 7 mwaka huu.












