China yazindua meli kubwa ya kubeba ndege za kivita

Vyombo vya habari vya serikali ya Chian vimesambaza picha za manowari hiyo ikiwa imerembeshwa kwa mapambo

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Vyombo vya habari vya serikali ya China vimesambaza picha za manowari hiyo ikiwa imerembeshwa kwa mapambo

China imetangaza kwamba imefanikiwa kuzindua manowari yake ya kwanza ya kujiundia yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita.

Meli hiyo ya kivita ina uzani wa tani 50,000.

Hatua hiyo inachukuliwa kama ishara ya karibuni zaidi ya kujiimarisha kwa taifa hilo katika nguvu za jeshi lake la majini.

Vyombo vya habari nchini China vinasema meli hiyo, ambayo inawezesha ndege kuruka na kutua juu yake, ilisafirishwa kutoka eneo ambalo ilikuwa ikiundiwa Dalian na kuwekwa baharini.

Inatarajiwa kuanza kazi rasmi mwaka 2020.

Kulinganisha meli kubwa za kivita za kubeba ndege
Maelezo ya picha, Kulinganisha meli kubwa za kivita za kubeba ndege
Meli hiyo ya kivita ilizinduliwa Dalian

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Meli hiyo ya kivita ilizinduliwa Dalian
Meli hiyo baada ya kung'oa nanga Dalian

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Meli hiyo baada ya kung'oa nanga Dalian

Meli pekee kubwa ya kubeba ndege inayomilikiwa na China ni meli ya Liaonong, ambayo ni meli ya enzi za muungano wa Usovieti iliyofanyiwa ukarabati.

China ilinunua meli hiyo kutoka kwa Ukraine.

Liaoning Dalian, 22 Sept 2012

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Meli ya kwanza ya kubeba ndege ya China kwa Liaoning ilinunuliwa kutoka Ukraine
Liaoning

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Meli ya Liaoning ilipokuwa inakabidhiwa rasmi kwa jeshi la wanamaji la China Septemba 2012