Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waasi wa FARC wafuta kundi hilo Colombia
Hatimaye Waasi wa FARC nchini Colombia wamemaliza rasmi uwepo wa kundi hilo kama kundi lililojihami kufuatia mzozo uliodumu nusu karne ambapo zaidi ya watu robo milioni waliuawa.
Akihutubia hafla karibu na mjini Mesetas, kiongozi wa FARC Rodrigo Londono, amesema kuwa shughuli ya kutwaa silaha kutoka kwa kundi hilo imekamilika hatua ambayo itabadilisha sura ya kundi hilo kuwa vugu vugu la kisiasa.
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos amesema taifa hilo linasherehekea siku ambayo silaha zilibadilishwa na maneno ya amani.
Mamia ya vipepeo waliachiliwa katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na maafisa wa serikali na waasi waliyovalia mavazi meupe kama ishara ya amani.