Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maziko salama yanusuru maisha Afrika Magharibi
Utafiti mpya wa hivi karibuni umebainisha kwamba mbinu ya maziko salama ulioanzishwa na chama cha msalaba mwekundu wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa ebola katika nchi tatu za Afrika Magharibi inaarifiwa umeokoa ama kuponya maisha ya maelfu ya watu.
Inakadiriwa kuwa watu wapatao elfu ishirini na tisa waliokuwa wameambukizwa ugonjwa wa ebola , walio wengi kutoka nchini Guinea, ierra Leone na Liberia, katika kipindi cha miaka ya 2013 na mwaka 2016.
Utafiti huo, umechapishwa katika jarida la PLOS lenye kujihusisha na masuala ya magonjwa ya kitropiki yaliyosahauliwa, limepongeza kazi kubwa iliyofanywa na chama cha msalaba mwekundu walijitolea kwa hali na mali kuzuia matukio zaidi ya elfu kumi .