Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
India: Msanii wa filamu India akosolewa kwa kumuonyesha miguu Narendra
Mchezaji filamu mashuhuri wa India Priyanka Chopra amekosolewa na watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa kuamua kuvaa gauni linaloonyesha miguu yake alipokutana na waziri mkuu wa India Narendra Modi.
Baadhi ya watumiaji wa Facebook walimwambia kuwa "alimkosea heshma " waziri mkuu".
Mchezaji filamu huyo ambaye hakuomba msamaha alijibu kauli hizo za ukosoaji kwa kutuma picha akiwa na mama yake wote wakiwa wamevalia gauni fupi, yenye maandishi "miguu ya siku".
Wachezaji filamu wengine wa India pia wamekuwa wakilengwa na hasira za wakosoaji wa mavazi wanayochagua kuyavaa.
Deepika Padukone wakati mmoja alililaumu gazeti la India kwa kuchapisha picha iliyoonyesha matiti yake mnamo 2014.
"NDIO! Mimi ni mwanamke. Nina matiti ! unashida!!??" Padukone aliutuma ujumbe wa twitter kwa gazeti. Wachezaji filamu wengine pia walijitokeza kumtetea.
Priyanka Chopra: Sipendi kulipwa pesa kidogo kuliko wanaume.
'nachukia kwamba tunaitwa Bollywood'
Utata ulianza baada ya Chopra, aliyecheza katika filamu ya the new Baywatch na katika kipindi cha marekani cha Quantico, alipotuma picha akiwa na Bwana Modi, akimshukuru "kwa kukuchukua muda licha ya kuwa na ratiba ya shughuli nyingi" kukutana naye mjini Berlin.
Sikufikiria hata kabla hata hivyo kwamba gauni la "kukosa heshima " litakuwa mada ya mazungumzo, huku wengi wakitoa kauli zao juu ya namna lili "mtusi " Bwana Modi na "wafuasi wake sugu."