Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Miili ya wanawake wanne ilipatikana eneo la Soweto mwishoni mwa wiki
Polisi nchini Afrika Kusini wanachunguza misururu mauaji ya wanawake wachanga kwenye mtaa wa Soweto mjini Johannesburg
Polisi wa Guateng wanafanya uchunguzi baada ya miili ya wanawake wanne kupatikana mwishoni mwa wiki eneo hilo.
Miili mitatu tayari imetambuliwa.
Bongeka Phungula na Popi Qwabe walitoweka siku ya Ijumaa na inaripotiwa kuwa pia walikuwa wamebakwa.
Mwili wa Lerato Moloi ulipatikana eneo la Naledi huko Soweto, huku mwili wa nne ukipatikana eneo la kutupwa taka.
Radio za Afrika Kusini zimepokea simu nyingi kutoka kwa raia wa Afika Kusini wanaoitaka serikali kuchukua hatua ya kupambana na uhalifu na kufanya jitihada za kuwalinda wanawake na watoto.