Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Dawa ya kifafa, hatari kwa wajawazito
Utafiti uliofanywa huko Ufaransa umebaini kuwa dawa ambayo imekuwa ikitumiwa kuwatibu wagonjwa wa maradhi ya kifafa, zinaweza pia kuathiri afya za watoto wachanga iwapo wanaotibiwa kwa dawa hizo wako katika umri wa kuweza kupata watoto.
Idara ya ufaransa inayohusika na viwango vya ubora wa dawa ( National Agency for the Safety of Medicines) imesema dawa hiyo valproate imepatikana kusababisha ulemavu wa aina fulani kwa watoto wanne kati 4100 wanaozaliwa ikiwa mama zao walipewa dawa hiyo hasa wakati wa uja uzito.
Dawa ya valproate ilianza kutumiwa nchini Ufaransa tangu miaka ya 60 na pia ingali inatumika sehemu nyingi duniani .
Sasa madaktari wa Ufaransa wameshauriwa wasiwape dawa hiyo wagonjwa wajawazito wala wasichana au akina mama walio katika umri wa kujifungua.
Baadhi wa waathiriwa wamesema Sanofi, kampuni wanaotengeza dawa hiyo, na maafisa wa afya wamejiburuza kuchukua hatua ilhali madhara ya valproate yalijulikana tangu miaka ya themanini.