Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis aongoza maelfu kwa ibada St Peter's Square

Chanzo cha picha, AFP
Maelfu ya mahujaji wamekusanyika Roma kushuhudia Papa Francis akiongoza ibada ya pasaka katika eneo la St Peter's Square.
Katika ibada ya kuamkia leo Papa Francis aliwahimiza waumini wasiwapuuze wahamiaji na maskini.
Ametoa ujumbe huu ukienda sambamba na shughuli wa kuwaoa zaidi ya watu 5,000 kutoka ngalawa mbovu zilizopatikana zikielea katika Ufuo wa Bahari ya Libya na Italia.
Papa Francis pia anatarajiwa kuzungumzia umuhimu wa mashauriano kati ya Madhehebu mbalimbali.
Matamshi hayo yanaonekana kulenga milipuko iliyotokea katika Kanisa la Coptic nchini Misri siku chache zilizopita.
Misa pia zilifanyika katika makanisa ya Coptic nchini Misri ambapo mashambulizi ya wiki iliyopita yalidaiwa kutekelezwa na Islamic State yaliwaua watu 45.

Chanzo cha picha, EPA

Chanzo cha picha, AFP

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, AFP








