Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Shirika la ujasusi Uingereza lakana kumdukua Trump
Mamlaka kuu ya mawasiliano ya kiintelijensia nchini Uingereza, G-C-H-Q, imetoa taarifa, kukanusha kuwa ilimdukua Bwana Trump wakati wa kampeini ya uchaguzi mkuu nchini Marekani.
Msemaji wa mamlaka hiyo anasema kuwa, madai yanayoashiria kuwa Uingereza ilitekeleza hatua hiyo , huku akinukuu tamko la msemaji wa Ikulu ya White House Bwana Sean Spicer, kama "matamshi ya kutamausha".
Madai hayo yaliyotolewa na mtangazaji mmoja wa Marekani, Andrew Napolitano, yalionekana hapo jana Alhamisi na msemaji wa Ikulu ya White House, Shon Spicer.
Rais Trump anadai kuwa mtangulizi wake Barrack Obama aliamuru kurekodiwa kwa mawasiliano ya simu zake zote.
Lakini viongozi wa vyama vya Republican na Democratic ndani ya kamati maalum ya ujasusi katika bunge la Seneti, wanasema hakuna dalili zozote zinazoonyesha kuwa Trump Tower ililengwa na majasusi wa nchi hiyo.