Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Trump amlaumu Obama kwa maandamano
Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaamini kuwa Barack Obama ndiye anahusika na maandamano dhidi ya uongozi wa Republican.
"Nafikiri Rais Obama anahusika kwa sababu ni watu wake wanaohusika kwenye maandamanohayo," Trump alikiambia kituo cha Fox News.
Trump hakutoa ushahidi wowote kwa madai yake na Obama bado hajajibu lolote.
Trump pia alizungumzia bajeti na masuala mengine.
Alipoulizwa kuhusu maandamano yanayohusu amri ya kusaka. alisema kuwa ni wafuasi wa Obama waliohusika.