Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wenger ashitakiwa na FA kwa utovu wa nidhamu
Chama cha soka cha England FA, kimemfungulia mashitaka ya utovu wa nidhamu meneja wa Arsenal Arsene Wenger, kwa madai ya kumkashifu refa na kumsukuma mwamuzi wa akiba.
Wenger alimsukuma mwamuzi wa akiba Anthony Taylor, na kutumia lugha mbaya katika mchezo ligi kuu ya England timu yake ilipocheza na Burnley.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika Wenger, aliomba radhi kwa kitendo alichofanya kilichopeleka kutolewa nje ya eneo ambalo huwa wanasimama makocha.
FA imempa kocha huyu mpaka muda mpaka siku ya Alhamisi saa 3 usiku kwa saa za Afika mashariki awe amewasilisha utetezi wake.
Hata hivyo Marefa wastaafu wa England, akiwemo Keith Hackett na Howard Webb, wametaka kocha huyu kupewa adhabu ya Kifungo kisichopungua michezo sita.