Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ndege yazindua viti vya wanawake pekee India
Kampuni ya ndege ya Air India hii leo inazindua ndege itakayokuwa na viti vya wanawake pekee kwa lengo la kukabiliana na unyanyasaji wa kingono .
Viti sita vitahifadhiwa wanawake, kwa ndege kadhaa.
Wanawake kadhaa akiwemo muhudumu mmoja wa ndege wamelalamikia ndege hiyo wakidai kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kingono na abiria wa kiume.
Mkuu wa muungano wa Abiria nchini humo amepinga mpango huo wa viti, akiutaja kuwa wa kiubaguzi.
Hatua ya kutenge viti kulingana na jinsia fulani sio jambo la kawaida kimataifa.