Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Buhari na matumaini ya kupatikana, wasichana wa Chibok
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anamatumaini juu ya kuachiliwa kwa wanafunzi wa kike 95 ambao bado wanashikiliwa na Boko Haram.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku elfu moja tangu kukamatwa na kundi hilo la wapiganaji, zaidi ya wasichana laki mbili kutoka mji wa Chibok, Aprili 2014, hali iliyosababisha, tukio hilo kufuatiliwa na vyombo vya habari vya kimataifa.
Zaidi ya wasichana 20 wameokolewa ama kupatikana toka wakati huo, ikiwemo mwingine mmoja aliyepatikana wiki iliyopita.
Katika Hotuba yake Rais Buhari amesema, Nigeria haitaacha kuwalilia watoto hao ambao bado wanashikiliwa.