Mshambuliaji avurumisha lori kwa wanajeshi Israel

Polisi wa Israil wanasema kuwa lori limevurumishwa mbele ya kundi la wanajeshi, mjini Jerusalem wakati wanajeshi hao wakiteremka kutoka basi.

Vyombo vya habari vya huko vinasema watu kama wane wameuwawa, na wengine kadha walijeruhiwa.

Inaarifiwa kuwa dereva wa lori alipigwa risasi na kuuwawa.

Polisi wanasema wanashuku kwamba lilikuwa shambulio la kigaidi.

Katika miezi 15 iliyopita, WaPalestina wamefanya mashambulio mengi dhidi ya Wa-Israil mara nyingi wakitumia visu.