Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kanda ya sauti ya Netanyahu yatolewa
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, anakabiliwa na shinikizo zaidi kufuatia madai ya ufisadi baada ya gazeti moja la Israel kuripoti kuwa polisi wana kanda ya sauti ya bwana Netanyahu ambayo inayaunga mkono madai hayo.
Bwaba Netanyahu amehojiwa mara mbili na polisi.
Awali Netanyahu alisema kuwa madai hayo hayana msingi wowote.
Gazeti la Haaretz hata hivyo limechapisha madai kuwa sasa polisi wana kanda ya sauti ambapo bwana Netanyahu anaripotiwa kusikika akiongea kwa njia ya simu na mfanyabiashara mmoja.
Hata hivyo madai hayo hayajathibitishwa rasmi.