Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Israel:Benjamin Netanyahu ahojiwa kwa tuhuma za rushwa
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anahojiwa na polisi kwa tuhuma za ruswa zinazomkabili.
Netanyahu amekana kuhusika katika jambo hilo, huku akisema malalamiko yanayotolewa kwa yeye kupokea zawadi kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali ni uongo.
Televisheni imewekwa nyumbani kwake kuonyesha wapelelezi hao wakimuhoji.
Tekelezo hilo ni kwa amri ya mwanasheria mkuu wa Israel.
Netanyahu na mke wake Sara wamehusishwa katika kashfa mbalimbali kipindi cha nyuma, ikiwemo tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za serikali.