Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kiongozi wa upinzani ashinda uchaguzi wa urais Gambia
Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Gambia amemtangaza mgombea wa upinzani Adama Barrow, kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.
Adama Barrow alipata kura 263,515 huku Rais Yahya Jammeh akipata kura 212,099.
Mwandishi mmoja wa habari kutoka shirika la Reuters anasema kuwa amezungumza na Adama Barrow aabaye amemuambia kuwa anasubiri simu ya kukubali kushindwa kutoka kwa bwana Jammeh.
Waziri wa masuala ya ndani nchini Gambia na mkuu wa polisi wamehutubia taifa wakitaka kuwepo utulivu.
Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Gambia amewaambia waandishi wa habari kuwa Rais Yahya Jammeh ambaye ameitawala nchi kwa miaka 22 baada ya kuingia madarakani kwa njia ya mapinduzi atakubali kushindwa.