Upinzani ''wapata ushindi wa mapema'' Gambia

Adama Barrow ameshinda mjini Banjul

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Adama Barrow ameshinda mjini Banjul

Matokeo ya kwanza kutoka uchaguzi wa urais nchini Gambia yanampa mgombea wa upanzani Adama Barrow ushindi dhidi ya Rais Yahya Jammeh.

Mwandishi wa BBC nchini Gambia anasema amepata thibitisho kuwa bwana Barrow ameshinda kwenye mji mku Banjul.

Hata hivyo ni chini ya asilimia 15 ya karibu wapiga kura 890,000 waliosajiliwa ndio imehesabiwa.

Bwana Jammeh ameitawala Gambia tangu mwaka 1994

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Bwana Jammeh ameitawala Gambia tangu mwaka 1994

Wanajeshi na polisi hii leo wameweka vituo vya ukaguzi kwenye barabara zinazoingia na kutoka mji mkuu.

Serikali ilizima huduma za mitandao na kufunga simu za kimataifa wakati uchaguzi ulikuwa ukiendelea.