Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Walioikimbia Cuba washerehekea kifo cha Castro, Urusi yaomboleza
Raia wa Cuba walioko uhamishoni Miami, ambao walisubiri kwa hamu kumalizika kwa utawla wa Muda mrefu wa Fidel Castro, wameimba na kucheza densi kwa shangwe kufuatia kifo chake licha ya mvua kunyesha.
Hata hivyo Rais wa Urusi Vladimir aliusifu ''urafiki wa kweli ''na rais wa Cuba Fidel Castro.
"Jina la mtu huyu maarufu kwakwa taifa ni ishara inayofaa kuangaliwa kama kielelezo cha enzi nzima katika historia ya dunia.
" Cuba iliyo huru naambayo yeye na washirika wake waliijenga imekuwa nchi mwanachama yenye ushawishi kwa jamii ya kimataifa na imekuwa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingi na watu.
"Fidel Castro alikuwa mkweli na rafiki mwaminifu kwa Urusi. Binafsi alianzisha mkataba mzuri wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano kati ya Urusi na Cuban relations, uliokuwa mkakati wa ushirikiano wa karibu kuwahi kushuhudiwa kote duniani.
"mtu huyu thabiti na mwenye busara mara kwa mara alikuwa na maono ya baadae kwa ujasiri. Alikuwa na sifa za juu za mwanasiasa, raia na mzalendo, alikuwa na uhakika na sababu ambayo alijitolea katika maisha yake yote.
"Kumbu kumbu yake itaishi daima katika mioyo ya ''Warusi''.