Maandamano ya kumpinga Rais yaendelea Korea Kusini

Maandamano yafanyika kwa wiki ya nne mfululizo Korea Kusini

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Maandamano yafanyika kwa wiki ya nne mfululizo Korea Kusini

Kwa wiki ya nne mfululizo maelfu ya watu wanaendelea kuandamana katika mji mkuu wa Seoul, nchini Korea Kusini, ili kumshinikiza Rais Park Guen Hye ajiuzulu.

Rais huyo amekataa kuitikia wito wao na kusalia madarakani.

Rais Park Guen Hye

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais Park Guen Hye

Hapo jana lijitokeza hadharani wa mara ya kwanza, zaidi ya wiki moja, kama ishara ya kuonyesha nia yake ya kutaka kuendelea kuhudumu kama rais.

Waandamanaji hao wameghadhabishwa na hatua yake ya kumruhusu mwanamke anayedaiwa kuwa rafiki yake wa karibu, Choi Soon-sil, kutumia ushawishi wake kufanya ulaghai.

Choi Soon-sil

Chanzo cha picha, AFP/GETTY

Maelezo ya picha, Choi Soon-sil

Mwanamke huyo kwa sasa anazuiliwa na maafisa wa usalama.