Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanasayansi: Ujangili bado ni janga sugu
Utafiti mpya unaonesha kuwa usafirishaji haramu wa pembe za ndovu zilizokamatwa unatokana na meno ya tembo ya hivi karibuni na si yale ya zamani yaliyohifadhiwa na serikali.
Ripoti hiyo ilichapishwa katika Chuo cha Taifa cha Sayansi huko Marekani.
Umoja wa Mataifa unasema asilimia tisini ya pembe za ndovu zilokamatwa kati ya mwaka 2002 na 2014 zilipatikana kutoka kwa wanyama waliokufa kipindi kisichozidi miaka mitatu kabla ya meno yao kuchukuliwa.
Wanasayansi wanasema jitihada zote ikiwemo kuonesha uhifadhi wa hali ya juu, kampeni mbalimbali, mikataba ya kimataifa na mamilioni ya dola ya misaada zaidi ya miongo kadhaa zimeshindwa kutatua tatizo la ujangili barani Afrika.
Shirika la kimatifa la umoja wa uhifadhi wa asili limesema kuwa katika kipindi cha mwezi Septemba kuwa idadi ya ndovu barani Afrika ilishuka kwa karibu asilimia ishirini kati ya 2006 na 2015, kwa sababu ya ongezeko la ujangili wa pembe za ndovu.