Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ethiopia yazilaumu Misri na Eritrea kwa kuchangia ghasia nchini mwake
Wazizi wa habari nchini Ethiopia anasema kuwa makundi nchini Eritrea na Misri yanachangia kuwepo ghasia ambazo zimesababisha kutangazwa hali ya harati ya miezi sita nchini humo.
Getachew Reda alisema kuwa vikundi vinawapa silaha na pesa makundi ya upinzanani. Chini ya hatua ya kutangaza hali ya hatati wanajeshi watatumwa kuzima maandamano.
Hii inafuatia miezu kadha ya maandamano ya kuipinga serikali yanayofanywa na makabil mawili makubwa zaidi nchini humo
Ghasia zimeongezeka tangua mwanzo wa mwezi huu wakati takriban watu 55 waliuawa wakati wa maandamano kwenye warsha moja ya dini ya kabila la Oromo.
Waziri huyo pia aliilaumu Eritrea ambayo Ethiopia imekuwa na mzozo wa mpaka nayo kwa muda mrefu.
Ethiopia pia imekuwa na tofauti na Misri baada ya uamuzi wa Ethiopia wa kujenga bwawa kwenye mto Nile