Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kimbunga Chaba chaua watu Korea Kusini, chaelekea Japan
Watu watano wameuawa na wengine wengi kuachwa bila makao baada ya kimbunga kwa jina Chaba kufika maeneo ya Korea Kusini kikiwa kimeandamana na upepo mkali na mvua.
Miji ya Busan na Ulsan kusini mwa nchi hiyo ndiyo iliyoathiriwa zaidi.
Kisiwa chenye hoteli za kitalii cha Jeju pia kimeathiriwa sana.
Shughuli za uchukuzi, viwanda, shule na uwanja mkuu wa ndege nchini humo zimekwama.
Picha zimeonesha maji ya mafuriko yakiwaa yamejaa barabarani.
Kimbunga hicho kwa sasa kinaelekea Japan ambapo idara ya utabiri wa hali ya hewa huko imetoa tahadhari na kusitisha safari za ndege.