Kimbunga Chaba chaua watu Korea Kusini, chaelekea Japan

Wahudumu wa feri waliokuwa wamerushwa majini na kimbunga hicho wakiokolewa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wahudumu wa feri waliokuwa wamerushwa majini na kimbunga hicho wakiokolewa

Watu watano wameuawa na wengine wengi kuachwa bila makao baada ya kimbunga kwa jina Chaba kufika maeneo ya Korea Kusini kikiwa kimeandamana na upepo mkali na mvua.

Miji ya Busan na Ulsan kusini mwa nchi hiyo ndiyo iliyoathiriwa zaidi.

Kisiwa chenye hoteli za kitalii cha Jeju pia kimeathiriwa sana.

Shughuli za uchukuzi, viwanda, shule na uwanja mkuu wa ndege nchini humo zimekwama.

Picha zimeonesha maji ya mafuriko yakiwaa yamejaa barabarani.

Kimbunga hicho kwa sasa kinaelekea Japan ambapo idara ya utabiri wa hali ya hewa huko imetoa tahadhari na kusitisha safari za ndege.

Changwon 2016.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Upepo ulifikia kasi ya 200km/h (124mph), na kung'oa miti Changwon
Busan, South Korea. 5 Oktoba 2016.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Barabara nyingi zimefurika maji
Ulsan, Korea Kusini 5 Oktoba 2016.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Watu wakiokolewa
Jeju, 5 Oktoba 2016.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Magari yaliyokuwa yameharibiwa na kimbunga kisiwani Jeju
Jeju, 4 Okotba 2016.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mawimbi yalitangulia upepo mkali ksiiwa cha Jeju
Mwimbi yaonekana yakiwa yameruka juu ya ukuta wa kukinga barabara kisiwa cha Jeju

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mwimbi yaonekana yakiwa yameruka juu ya ukuta wa kukinga barabara kisiwa cha Jeju