Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Watoto wa Tanzania wana afya nzuri ya maungo duniani
Taifa la Tanzania ndilo lenye watoto wenye afya nzuri ya maungo duniani, kulingana na utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Australia.
Viwango vya afya ya maungo ya watoto milioni 1.1 walio kati ya umri wa miaka tisa hadi 17 kutoka mataifa 50 vilifanyiwa ukaguzi.
Watoto hao walifanyiwa zoezi la kukimbia umbali wa mita 20,ambalo hukagua afya yao ya maungo.
Grant Tomkinson, mmoja ya watafiti wakuu wa chuo cha Kusini mwa Australia ameiambia BBC kwamba watoto wa Tanzania waliibuka washindi kutokana na utendaji wao.