Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Choo kilichotengezwa kwa dhahabu kutumika na umma
Raia wako huru kutumia fedha zao kidogo ili kupata huduma ya choo kilichotengezwa na dhahabu katika jumba la makumbusho la Guggenheim.
Msanii kutoka Italy,Maurizio Cattelan alijenga choo hicho kwa kutumia carat 18 za dhahabu na kukiita choo hicho Marekani.
Choo hicho cha maonyesho kimewekwa katika msala wa kuogea wa Guggenheim kulingana na the New Yorker.
Jumba hilo la makumbusho limekitaja choo hicho kuwa kazi nzuri.
Choo hicho cha dhahabu kilijengwa katika choo chengine kinachotumiwa na jinsia zote mbili.
Wageni wanaolipa kiingilio cha jumba hilo la makumbusho wataweza kukitumia wanavyotaka.
Choo hicho kinalenga kuwapa fursa raia wa tabaka la chini kujifurahisha katika mandhari ambayo hutumiwa na matajiri pekee.