Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tofauti kati ya wanaume na wanawake ni hasara kwa bara Afrika
Umoja wa Mataifa unasema, nchi za Afrika Kusini ya Sahara, zinapata hasara ya dola kama bilioni 95 kila mwaka, kwa sababu ya tafauti baina ya wanaume na wanawake.
Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Helen Clark, anasema katika sehemu nyingi za Afrika, wanawake wanapata tabu kukopa fedha, kwa sababu hawana ardhi ya kuweka dhamana.
Hii inamaanisha hawawezi kununua mbegu nzuri na mbolea, na kwa hivyo hawawezi kuzalisha mazao kwa wingi.
Bi Clark anasema, tofauti zikiondolewa, basi uchumi wa Afrika utakuwa kwa kiwango kikubwa zaidi.