Korea Kaskazini yamzungumzia balozi aliyekimbia nchi

Chanzo cha picha, Getty Images
Korea Kaskazini imemshutumu mwanabalozi wake aliyekimbilia Korea Kusini hivi karibuni, kwamba mhalifu.
Katika matamshi ya kwanza, tangu balozi huyo kukimbia, shirika la habari la Korea Kaskazini, lilimuelezea mwanabalozi huyo kuwa mtu duni kabisa.
Lilisema mkimbizi huyo alikuwa akichunguzwa kwa ubadhirifu wa mali ya taifa, na kuuza siri za nchi.
Awali juma hili, Korea Kusini ilitangaza kwamba Thae Yong-ho, ambaye alikuwa naibu balozi wa Korea Kaskazini mjini London, aliwasili Korea Kusini na familia yake.
Anafikiriwa kuwa mwanabalozi wa cheo cha juu kabisa wa Korea Kaskazini, kuwahi kukimbia.








