'Marafiki wenye uadui': Uhusiano wa Trump na Ulaya wakati huu unaweza kuwa tofauti sana

Na Katya Adler
Mhariri Ulaya
"Ni jambo la kipuuzi! Tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu. Nchi inahisi kuwa na huzuni. Uchumi wetu unayumba... Lakini vyombo vingi vya habari vya Ujerumani vinaonekana kuandika taarifa zinazomhusu Trump, Trump, Trump!"
Iris Mühler, mwalimu wa uhandisi kaskazini mashariki mwa Ujerumani ni mmoja wa wapiga kura kadhaa ambao nimekuwa nikizungumza nao kabla ya uchaguzi mdogo wa Februari. Si peke yake mwenye mtazamo huu.
Licha ya kukabiliwa na matatizo yake ya ndani Ulaya imekuwa ikimfuatilia sana Trump tangu aliposhinda uchaguzi wa rais wa Marekani mnamo Novemba.

Chanzo cha picha, Getty Images
Bara hilo lilikuwa na safari iliyokuwa na vizingiti mara ya mwisho alipokuwa Ikulu ya White House. Wengi wanahofia kuwa utawala wa Trump wa 2.0 unaweza kuwa mbaya zaidi. Na mataifa ya Ulaya tayari yanapambana na matatizo yao wenyewe.
Ufaransa na Ujerumani zinakabiliwa na matatizo ya kisiasa na kiuchumi, EU kwa ujumla iko nyuma ya China na Marekani katika suala la ushindani, wakati nchini Uingereza, huduma za umma ziko katika hali mbaya.
Kwa hivyo: je, bara hilo liko tayari kwa Donald Trump?
Mfanyabiashara anayekataa ushirikiano
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Linapokuja suala la biashara na ulinzi, Trump anatenda zaidi kama mfanyabiashara wa shughuli kuliko mtu wa Marekani ambaye anatoa ushirikiano wa nchi zinazounganishwa na Bahari ya Atlantiki kwa biasahara tangu Vita vya Pili vya Dunia.
"Haamini katika ushirikiano wa ushindani," Kansela wa zamani wa Ujerumani Angela Merkel aliniambia. Alimshuhudia Trump mara ya mwisho alipokuwa madarakani na kuhitimisha kuwa anautazama ulimwengu kwa njia ya washindi na walioshindwa.
Anaamini kwamba Ulaya imeitumia Marekani kujinufaisha kwa miaka na hilo linapaswa kukoma.
Viongozi barani Ulaya wametazama wazi wiki hizi za hivi karibuni tangu Trump aliposhinda uchaguzi wa rais wa Marekani, kwa mara ya pili. Amechagua kuwalaumu hadharani washirika wake barani Ulaya na Canada, badala ya kuzingatia maslahi kwa wale anaowatambua kama tisho la kimkakati, kama China.
Trump alielezea uwezekano wa kuachana na Nato - muungano wa kijeshi ambao Ulaya imetegemea kwa usalama wake kwa miongo kadhaa. Amesema "ataihimiza" Urusi kufanya "chochote wanachotaka" na washirika wa Ulaya ikiwa "hawatalipa" gharama zaidi na kuongeza matumizi yao ya ulinzi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Linapokuja suala la biashara, ni wazi Trump ana hasira na EU sasa sawa na aliyokuwa nayo wakati wa muhula wake wa kwanza mamlakani.
Muungano huo wa Ulaya unauza zaidi kwa Marekani kuliko inavyoagiza kutoka Marekani. Mnamo Januari 2022, biashara ya ziada ilikuwa na thamani ya € 15.4 bilioni (£ 13 bilioni).
Majibu ya Donald Trump ni yapi?... Anasema ataweka ushuru wa jumla kwa bidhaa zote za kigeni zinazoingizwa kutoka nje kwa asilimia 10-20, na hata ushuru wa juu zaidi kwa bidhaa fulani kama magari.
Hiyo ni hali ya maafa kwa Ujerumani, ambayo inategemea mauzo ya nje na hasa sekta ya magari. Uchumi wake tayari umeporomoka - mwaka jana, ulipungua kwa 0.2%.
Kama uchumi mkubwa katika eneo la sarafu ya Euro-eurozone, matatizo ya kifedha nchini Ujerumani yanahatarisha kuathiri sarafu kwa ujumla.
Ujerumani iko 'juu kwenye ya orodha ya Trump'
Merkel amesema wakati alipokuwa rais mara ya mwisho, Trump alionekana kuwa na msimamo huo kwa Ujerumani.
Ian Bond, naibu mkurugenzi wa Kituo cha Mageuzi ya Ulaya, anaamini nchi hiyo itabaki kuwa "juu ya orodha ya Trump (Ulaya).
"Kile alichosema zamani ni mambo kama, hataki kuona Mercedes-Benz yoyote kwenye mitaa ya New York. Sasa, hii ni aina ya karanga, kwa sababu, kwa kweli, mengi ya magari ya Mercedes-Benz ambayo unaona kwenye mitaa ya New York yanatengenezwa huko Alabama, ambapo Mercedes ina kiwanda kikubwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Mara nyingi amekuwa na chuki zaidi kwa Ujerumani kuliko nchi nyingine yoyote barani Ulaya. Inaweza kuwa rahisi kidogo kwa Ujerumani na serikali mpya na ya kihafidhina zaidi (baada ya uchaguzi mkuu ujao)."
Uingereza inatarajia kuepuka ushuru wa Trump kwani haina usawa wa biashara na Marekani, lakini inaweza kuathirika iwapo kutakuwa na vita vya kibiashara kati ya Marekani na Ulaya.
Je, Ulaya imejiandaa vipi?
Mtindo wa Trump wa kunyanyasa hauwezi kuwa wa kushangaza kwa washirika wake baada ya muhula wake wa kwanza katika ikulu ya White House. Kibarua halisi kwa Ulaya sasa ni kutotabirika kwake: Ni kiasi gani cha majigambo na vitisho na ni kiasi gani cha ahadi na hatua?
Ian Lesser, makamu wa rais katika mfuko wa Ujerumani wa Marshall Fund of the United States , anaamini vitisho vya ushuru wa Trump ni vya kweli na kwamba Ulaya iko mbali na tayari.
"Hawako tayari, hakuna mtu wa kweli. Njia hii tofauti sana ya biashara ya kimataifa inavuruga misingi mingi ya uchumi wa kimataifa, ambao umebadilika kwa miongo kadhaa."

Chanzo cha picha, Getty Images
Tume ya Ulaya inadai kuwa iko tayari kwa hatua yoyote ya Trump atakaporudi White House. Ni nguvu kubwa ya biashara katika hatua ya ulimwengu.
Lakini Bwana Lesser anasema athari kubwa zaidi kwa Ulaya inaweza kutokea iwapo Trump ataanzisha vita vya kibiashara dhidi ya China.
Hiyo inaweza kusababisha usumbufu wa ugavi kwa Ulaya na Beijing kutupa bidhaa za bei rahisi zaidi kwenye masoko ya Ulaya, kwa uharibifu wa biashara za ndani.
"Kwa Ulaya athari ni mara mbili : zitokanazo na kile Amerika inachoweza kufanya na kisha kile China itakafanya katika kujibu."
Biashara, ulinzi na sababu ya Musk
Kinacholeta utata zaidi ni kwamba biashara na ulinzi sio masuala tofauti kwa Trump na utawala wake.
Hivi karibuni alikataa kuondoa hatua za kiuchumi na / au kijeshi dhidi ya EU na mwanachama wa Nato Denmark endapo haitakabidhi eneo la Greenland kwa Marekani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hivi karibuni, Bw Musk pia alionyesha nia ya kuchukua msimamo katika siasa za Ulaya. Alianzisha mashambulizi ya mara kwa mara mtandaoni dhidi ya viongozi wa mrengo wa kati wa kushoto wa Ulaya Sir Keir Starmer nchini Uingereza na Kansela wa Ujerumani anayeondoka Olaf Scholz. Musk aliandika kwenye mtandao wa X kwamba chama cha AfD kinachopinga uhamiaji ndio matumaini pekee ya Ujerumani.
Hii iliwashangaza wengi barani Ulaya lakini wapiga kura wanapendekeza kuwa machapisho yenye utata ya Musk hayana ushawishi mkubwa kwa maoni ya umma ya Ulaya.
Trump na Musk hawaaminiki sana barani Ulaya, kama ilivyoonyeshwa wazi katika kura mpya ya maoni iliyoagizwa na Baraza la Ulaya la Mahusiano ya Nje, yenye kichwa EU na maoni ya umma ya ulimwengu baada ya uchaguzi wa Marekani.
Kutoka sifa za ubinafsi hadi kuonyesha fedha
Mwishowe, viongozi tofauti wa Ulaya wana njia tofauti za "kumzuia Trump," huku wandaniwakielezea kuwa kulikuwa na majaribio ya kufanya hilo. Baadhi wakielezea kwamba kujidai kwa Trump ni katika matamshi pekee.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ni mtaalamu kwa hili. Alikuwa mmoja wa viongozi wa kwanza duniani kumpongeza Trump katika mitandao ya kijamii baada ya kuchaguliwa tena mwezi Novemba na alimwalika kwa haraka kuhudhuria ufunguzi wa kanisa kuu la Notre Dame mjini Paris.
Wakati alipokuwa wa kwanza katika Ikulu ya White House, Rais Macron alimfurahisha Trump kama mgeni wa heshima katika maonyesho ya kila mwaka ya nguvu za kijeshi za Siku ya Bastille huko Paris.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uingereza, wakati huo huo, inajua Trump anauhusiano wa karibu na Uskochi , ambapo mama yake anatoka, na kwa Familia ya Kifalme ya Uingereza.
Alitegemea kuhudhuria karamu ya serikali na Malkia Elizabeth II wa sasa mnamo 2019. Alimsifu Prince William baada ya kukaa naye msimu huu wa vuli.
Mkuu wa Benki Kuu ya Ulaya (ECB), Christine Lagarde, amewashauri viongozi wa Ulaya kujadiliana na Trump badala ya kulipiza kisasi dhidi ya ushuru wake uliopendekezwa.
Ursula von der Leyen, rais wa Tume ya Ulaya, anazungumza juu ya kununua zaidi (gharama) za gesi ya asili ya Marekani (LNG) kama sehemu ya juhudi za Ulaya za kupanua usambazaji wake wa nishati.
Imekuwa ikiacha kutegemea gesi ya bei nafuu ya Urusi tangu Kremlin ilipoanzisha uvamizi wake mkubwa wa Ukraine.
Vyanzo katika tume pia vinazungumzia uwezekano wa kununua bidhaa zaidi za kilimo za Marekani na silaha.
Je, Ulaya inapaswa kuwa ya kujitegemea zaidi?
Macron, wakati huo huo, kwa muda mrefu amekuwa akitetea kile anachokiita "uhuru wa kimkakati" - kimsingi Ulaya kujifunza kuwa ya kujitegemea zaidi, ili kuishi.
"Ulaya... inaweza kufa na hiyo inategemea kabisa uchaguzi wetu," alisema msimu huu wa majira ya kiangazi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Covid ilionyesha jinsi Ulaya ilivyokuwa tegemezi kwa uagizaji wa China, kama dawa. Uvamizi wa Vladimir Putin wa Ukraine ulifichua utegemezi wa Ulaya wa ya nishati ya Urusi.
Macron sasa anatoa tahadhari kuhusu Marekani: "Marekani ina vipaumbele viwili. Marekani kwanza, na hiyo ni halali, na suala la China, pili. Na suala la Ulaya sio kipaumbele cha kijiografia kwa miaka ijayo na miongo."
Kurejea kwa Trump katika ikulu ya White House kunawafanya viongozi wa Ulaya kufikiria kuhusu udhaifu wa bara.
Swali kubwa kuhusu ulinzi
Emmanuel Macron anataka sera ya ulinzi wa viwanda ya EU. Anasema vita nchini Ukraine vilionyesha kuwa "kugawanyika kwetu ni udhaifu... Wakati mwingine tumejigundua wenyewe, kama Wazungu, kwamba bunduki zetu hazikuwa sawa, kwamba makombora yetu hayakufanana."

Chanzo cha picha, Getty Images
Ulaya ina wasiwasi kwamba Trump hatataka kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa misaada ya kijeshi kwa Ukraine kama ilivyokuwa chini ya utawala wa Biden.
Mwezi ujao, viongozi wa EU wameialika Uingereza - moja ya nguvu mbili kubwa za kijeshi za Ulaya - kwenye mkutano usio rasmi kujadili kufanya kazi pamoja vizuri juu ya usalama na ulinzi.
Mkuu wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya na waziri mkuu wa zamani wa Estonia Kaja Kallas, anaamini umoja wa Ulaya unahitajika. "Tunahitaji kufanya kazi kwa umoja. Kwa hiyo, sisi ni wenye nguvu. Kwa hiyo, sisi pia tuko katika hatua ya kimataifa."
Je, Ulaya ya leo ni dhaifu na yenye mpasuko zaidi ?
Kuna wachambuzi ambao wanasema Ulaya iko katika hali dhaifu zaidi, iliyovunjika zaidi kukabiliana na utawala wa pili wa Trump kuliko ilivyokuwa mwaka 2016 wakati alipochaguliwa kwa mara ya kwanza.
Naweza kusema jibu la hilo ni ndiyo. Lakini pia hapana.
Ndiyo - kama ilivyojadiliwa, ukuaji wa uchumi ni wa kizembe na siasa ni tete.
Vyama vya kizalendo vya kizalendo vya Ulaya vinapata nguvu katika nchi nyingi za Ulaya. Baadhi, kama chama cha Ujerumani cha AfD, ni havina misimamo mikali kwa Moscow - wakati wengine kama Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni wanaweza kujaribiwa kuweka kipaumbele mahusiano ya biashara ya kupitia Baharai ya Atlantiki na Trump badala ya umoja wa Ulaya.
Lakini jihadharini na kuangalia nyuma Ulaya wakati Trump alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa rais.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baadhi ya watu wanaamini Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, huenda akatanguliza uhusiano imara na Donald Trump juu ya umoja wa Ulaya.
Kifedha, Ulaya ya kaskazini ilikuwa ikifanya vizuri zaidi kuliko ilivyo sasa, lakini, kwa suala la umja, bara hilo liligawanyika sana nyuma ya mgogoro wa wahamiaji mnamo 2015.
Baada ya Brexit Uingereza inaonekana na EU kama mshirika wa karibu ambaye anashiriki maadili sawa katika ulimwengu unaokabiliwa na tisho , China yenye tamaa, Urusi ya upanuzi na rais wa Marekani asiyetabirika, anayeingia mamlakani.
Nato, ingawa ina wasiwasi juu ya ahadi ya Trump kwa muungano huo, imeimarishwa kijeshi na kijiografia na Sweden na jirani wa Urusi Finland kuwa wanachama kufuatia uvamizi kamili wa Kremlin wa Ukraine.
Labda, labda tu, Trump ataona tofauti chache ambazo zinamsumbua na kumkasirisha kuhusu Ulaya wakati huu.
Je, ni Ulaya ambayo viongozi wake pia wanamtetea Trump, licha ya vitisho na usaliti, ikiwa wanahisi anavuka mstari - iwe ni kuhusu haki za binadamu, uhuru wa kujieleza au kushirikiana na madikteta? Ni ukurasa wa uhusiano kati ya Ulaya na Marekani unasubiriwa kuandikwa.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












