Anthony Zurcher: Ahadi na hatari ya hotuba ya Trump

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Trump akitia saini maagizo ya rais Jumatatu jioni baada ya kuapishwa.
Muda wa kusoma: Dakika 4

Donald Trump, ambaye alirejea madarakani kutokana na wimbi la kutoridhika na hali kwa wapiga kura, aliahidi mpya ya "enzi ya dhahabu" kwa Marekani katika hotuba ya kuapishwa kwake.

Hotuba hiyo ilikuwa na mchanganyiko wa ahadi na utata ambayo alisisitiza kuhusu baadhi ya fursa na changamoto ambazo rais mpya atakabiliana nazo katika muhula wake wa pili madarakani.

Alizingatia hasa uhamiaji na uchumi, masuala ambayo kura za maoni zinaonyesha wapiga kura wa Marekani waliyajali zaidi mwaka jana walipopiga kura ya urais.

Pia aliahidi kumaliza mipango ya serikali ya utofauti na akabainisha kuwa sera rasmi ya Marekani itatambua jinsia mbili tu, ya kike na ya kiume.

Mstari huo wa mwisho wa hotuba yake uliibua hisia za shauku katika jengo la Capitol na shangwe kubwa kutoka kwa umati wa wafuasi wake waliokusanyika katika uwanja wa michezo ulio karibu.

Ni ishara kwamba masuala ya kitamaduni ambayo alitofautiana kwa kiasi kikubwa na Democrats katika uchaguzi wa mwaka jana - yataendelea kuwa moja ya njia yenye nguvu zaidi ya Trump yatakayomuunganisha rais mpya anaunganisha na wafuasi wake wa mashinani.

Kabla ya kueleza ni nini enzi hii mpya itahusisha, hata hivyo, Trump alichora picha nyeusi ya hali ya kisiasa ya sasa ya Marekani.

Wakati mtangulizi wake, Joe Biden, na Wademocrat wengine wakiwa na nyuso zisizoonyesha hisia upande mmoja, Trump alisema serikali inakabiliwa na "mgogoro wa uaminifu". Alilaani "silaha za kikatili, za vurugu na zisizo za haki" za wizara ya sheria ya Marekani, ambayo ilikuwa imechunguza na kujaribu kumshtaki kwa kupinga matokeo ya uchaguzi wa 2020.

Alidai kuwa na mamlakaya kubadilisha "usaliti wa kutisha" na kukemea "kuanzishwa kwa siasa kali na ufisadi" ambavyo alisema vyviliwanyang'anya mamlaka ya nguvu na utajiri kutoka raia wa Marekani.

Hotuba ya trump ilikuwa ni ya aina ya matamshi ambayo amekuwa akiyatoa kwa kipindi cha muongo mmoja ya watu wenye msimamo mkali, yanayopinga ubaguzi.

Tofauti na wakati Trump alipoanza kupanda kwa nguvu za kisiasa za Marekani mwaka 2015, Trump hatahivyo anawakilisha kuanzishwa kwa sasa kama mtu yeyote.

Walioketi nyuma yake walikuwa ni baadhi ya matajiri wakuu zaidi duniani , na wenye ushawishi mkubwa, na viongozi wakuu wa makampuni makubwa duniani.

Unaweza pia kusoma:
g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos na mkewe Lauren Sanchez walichangamana na mabilionea wengine wa teknolojia wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Trump
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Katika siku ya kuapishwa kwake, Trump alikuwa na mipango. Wasaidizi wake wameahidi mamia ya hatua za kiutendaji, katika masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uhamiaji, nishati, biashara, elimu na masuala muhimu ya kitamaduni.

Katika hotuba yake ya uzinduzi, alielezea machache miongoni mwake. Aliahidi kutangaza dharura za kitaifa juu ya nishati na uhamiaji, ili kumruhusu kuweka jeshi la Marekani kwenye mpaka, kupunguzwa kwa kiasi kikubwa haki za wanaotafuta hifadhi na kufungua tena sehemu kubwa ya ardhi ya shirikisho kwa uchimbaji wa mafuta. Alirudia ahadi yake ya kubadilisha jina la Ghuba ya Mexico kuwa Ghuba ya Marekani "Gulf of America" na kuchukua Mfereji wa Panama.

Alitoa madai yasiyo na msingi kwamba China ilikuwa inaendesha njia muhimu ya maji na kusema kuwa meli za Marekani, ikiwa ni pamoja na meli za majini, zimekuwa zikilipa za juu sana za usafiri – huenda kikawa ni kidokezo cha lengo halisi katika mazungumzo ya baadaye na serikali ya Panama.

"Marekani kwa mara nyingine tena itajiona kuwa taifa linalokua," alisema, akiahidi kuongeza utajiri wa Marekani na kupanua "eneo letu".

Hatua hiyo ya mwisho inaweza kuwavutia washirika wa Marekani, ambao tayari wamekuwa na wasiwasi na nia ya Trump ya kutaka kuinunua Greenland na kuitaka Canada kuwa taifa la 51 la Marekani.

Katika kampeni, na katika hotuba hii, Trump alitoa mfululizo wa ahadi kubwa. Sasa kwa kuwa yeye ni rais, anakabiliwa na changamoto ya kuonyesha iwapo "enzi ya dhahabu" anayoimaanisha ni ya kweli.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi