Vita vya Ukraine: Maswali 5 muhimu ya kuchambua nini kinaweza kutokea 2023

Je, 2023 itakuwa vipi kwa watu wa Ukraine wanaokabiliwa na vita?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Je, 2023 itakuwa vipi kwa watu wa Ukraine wanaokabiliwa na vita?

Baada ya miezi kadhaa ya mapigano makali na hasara kubwa kwa pande zote mbili, je, kuna dalili kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin amechoshwa na mapambano hayo?

Steve Rosenberg: "Hakuna uchovu, hapana - hakuna ishara. Kutokana na hotuba ya Mwaka Mpya ya Rais wa Urusi, tumepata wazo nzuri la wapi Vladimir Putin yuko hivi sasa, anafikiria nini, na wapi anataka kuipeleka Urusi mwa 2023.

 Rais Vladimir Putin akitoa hotuba yake ya mwaka mpya akiwa amezungukwa na watu waliovalia sare

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Vladimir Putin akitoa hotuba yake ya mwaka mpya akiwa amezungukwa na watu waliovalia sare

"Ukiweka kando kile alichosema, nadhani picha zilisema yote, kwa kweli, kwa sababu alipokuwa akitoa hotuba yake, waliosimama nyuma yake wakiwa na uso wa huzuni walikuwa wanaume na wanawake waliovalia sare.

Ilikuwa picha ya kushangaza ambayo iliambia taifa. : 'Hii ni nchi yako sasa. Hii ni Urusi ya 2023 - nchi iliyo kwenye vita.'

Ingawa bado haviiti vita, [ni] nchi ambayo kila kitu kinalenga kupata ushindi wa kijeshi dhidi ya Ukraine, dhidi ya Nato, dhidi ya nchi za Magharibi na ambapo kila mtu hapa anatarajiwa kuunga mkono malengo haya na kuwa tayari kufikia mwisho - hakuna mjadala, hakuna majadiliano juu ya hilo, simama karibu na bendera yako, na mimi kiongozi wako.

Hizo zilikuwa taswira tu na unaposikiliza kile alichosema hasa - hakuna ishara ya kutafuta amani na maelewano, au hata nia ya kusema 'tutafute njia ya kutoa kwenye zogo hili'.

Huyu ni rais mwenye nia ya kupata ushindi, ama kwa sababu anaamini kuwa ushindi unawezekana, au kwa sababu Putin anajua yuko kwenye kina kirefu sasa hivi na kwamba hakuna njia ya kurudinyuma ...ana chaguo moja tu nalo ni kusonga mbele kwa matumaini kwamba kitu kitabadilika kwa manufaa yake."

Vipi kuhusu Waukraine? Je, wataendelea?

Mifumo ya kisasa ya silaha za Marekani na Nato kama vile Mfumo wa Roketi wa Kusonga Zaidi (Himars) umesaidia sana juhudi za vita za Ukraine.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mifumo ya kisasa ya silaha za Marekani na Nato kama vile Mfumo wa Roketi wa Kusonga Zaidi (Himars) umesaidia sana juhudi za vita za Ukraine.

Jeremy Bowen: "[Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amekuwa akizungumzia] kurudisha ardhi yao iliyopotea - na katika hilo anajumuisha Crimea, jimbo kubwa ambalo walipoteza mnamo mwaka 2014.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Sasa Zelensky amejionyesha kuwa kiongozi bora wa vita, lakini swali la nini wanaweza kufikia kijeshi linategemea msaada wa Nato na haswa kile wanachopata kutoka Marekani- silaha za hali ya juu walizokuwa nazo kama mfumo wa makombora wa Himars yamefanya uharibifu mkubwa.

Lakini Rais Biden huko Washington amekuwa akitumia njia ya busara na makini ambayo kimsingi ni kwamba Ukraine haiwezi kuruhusiwa kupoteza na lazima iungwe mkono ili iweze kupata ushindi, lakini usiisukume Urusi ili kuzuia isitimize vitisho vya vyake vya kutimia silaha za nyuklia.

Sasa, Waukraine wanatambua kwamba kurejesha ardhi yao, wanahitaji mengi zaidi ya mashambulio ya nguvu.

Nilipokuwa Ukraine mara ya mwisho wakati Warusi walipokuwa wakitoka katika jiji la kusini la Kherson, makamanda wote katika eneo hilo niliozungumza nao walisema, ili washinde vita kwa njia wanayotaka, wanahitaji mengi. , nguvu zaidi ya mashambulizi katika suala la mizinga ya kisasa, kwa upande wa ndege na hivyo ndivyo vitu ambavyo hawapati."

Je, msaada wa kigeni kwa Ukraine utapungua?

Mnamo Novemba, Jenerali wa Marekani Mark Milley alionyesha mashaka kwamba Crimea inaweza kukombolewa tena na Waukraine

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mnamo Novemba, Jenerali wa Marekani Mark Milley alionyesha mashaka kwamba Crimea inaweza kukombolewa tena na Waukraine

Rosenberg: "Nadhani hiyo ni sehemu ya hesabu ya [Putin], kwa sababu jinsi mambo yalivyomwendea vibaya tangu Februari 24 mwaka jana, bado anaamini ana kadi kali na anaamini nadhani nchi za Magharibi zitachoshwa na vita hivi na kupunguza msaada wake kwa Ukraine.

Kuna kila aina ya uvumi unaoibuka kwamba kunaweza kuwa na wimbi jipya la uhamasishaji nchini Urusi, kuna mazungumzo juu ya uwezekano wa kukereka kwa jeshi la Urusi. Mamlaka zimekuwa na furaha na kuzungumza juu ya ushindi."

Bowen: "Mnamo Novemba, mwenyekiti wa Wakuu wa Pamoja wa Wafanyakazi wa Marekani, Jenerali Mark Milley, alisema kuwa kutwaa tena Crimea itakuwa vigumu na labda alikuwa akimaanisha, nadhani, si jambo la kuhitajika."

Vipi kuhusu msaada nchini Urusi?

Rosenberg: "Kuna mgongano kati ya ujumbe kutoka Kremlin na hali halisi kwa sasa. Kwa upande mmoja, una Putin akihamasisha taifa katika hotuba ya Mwaka Mpya, kutangaza ushindi, na dakika chache baadaye - kiuhalisi - Ukraine yafanya shambulio baya la roketi dhidi ys kambi ya kijeshi ya Makiivka.

 Baada ya mateso mengi, Jeremy Bowen anaamini kuwa uongozi wa Ukraine hauko katika hali ya kulazimishwa kufanya makubaliano

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baada ya mateso mengi, Jeremy Bowen anaamini kuwa uongozi wa Ukraine hauko katika hali ya kulazimishwa kufanya makubaliano

Ninazungumza juu ya ujumbe kinzani, lakini kile tunachoshuhudia ni halii hii sambamba ambao tumekuwa tukizungumza kwa karibu mwaka sasa.

Ikiwa unataka kujua Urusi ya 2023 ni nini, vuka George Orwell na Lewis Carroll na utapata wazo halisi.

Ni mchanganyiko wa ajabu sana wa 1984 na [Alice] Kupitia taswira inayoashiria kila kitu kiko juu chini na nyuma mbele na nje: vita ni amani, ujinga ni nguvu.

Kremlin imeunda aina hii ya ukweli mbadala ambayo inakuza na kuendeleza kutoka usiku na mchana katika vyombo vya habari vya serikali, ambapo Urusi inaonyeshwa kama mwathirika na Ukraine na nchi za Magharibi ni wavamizi walioanzisha vita."

Je, upande wowote uko tayari kuafikia makubaliano?

Bowen: "Je, kuna eneo la kutua la aina fulani, hivi sasa kwa ajili ya mazungumzo? Sidhani hivyo, kwa sababu Putin ama anaamini kuwa anaweza kushinda au anaamini kwamba lazima aendelee.

Na Waukraine wanaamini kwamba wanaweza kushinda na licha ya kupoteza damu nyingi na kupata uharibifu mkubwa hawatakubali kuingizwa kwenye makubaliano ambayo hawataki.

Msimamo wa Zelensky umebadilika tangu mwanzo wa vita. Kabla ya Machi katika wiki za kwanza wakati mji mkuu ulionekana kuwa chini ya tishio la kweli kutoka kwa Warusi, alikuwa akisema mambo kama: "Maisha ni muhimu, muhimu zaidi, labda, kuliko eneo". Sasa anasema wanataka kila sehemu ya nchi yake iliyonyakuliwa irudishwe na kama wanataka kuzungumza, kumaanisha Warusi wanapaswa kuondoka katika ardhi yao."